August 28, 2018




Aina ya uchezaji wa Shiza Kichuya katika kikosi cha Simba, umekuwa gumza wengi wakiona ni tofauti na ilivyokuwa.

Kocha Patrick Aussems anaonekana kumtumia Kichuya kama Free Role, yaani mchezaji mwenye uhuru zaidi wa kupandisha mashambulizi.
Katika mjadala ulioanzishwa na Blog ya SALEHJEMBE na wapenda mpira kutuma maoni yao, inaonekana wengi zaidi wamefurahishwa.

Wengi ya waliochangia wamesema Kichuya ana ubunifu na Kocha Aussems amekuwa mbunifu zaidi kuliona hilo la Kichuya na atawasaidia.

Lakini kwa wachache wanaoona si sawa, wanaamini Kichuya angetumika sawa na viungo wengine ili naye asaidie suala la ukabaji wanapokuwa wanashambuliwa.
Kichuya amekuwa akitumika zaidi katika mashambulizi huku mipira mingi akipewa yeye.

Utawaona viungo wenzake kila wanapokuwa na mpira humkabidhi na yeye kuanza kupanga mashambulizi.

Tayari Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, wameshinda mechi zao mbili za kwanza wakianza kwa kuitungua Prisons kwa bao 1-0 na baadaye Mbeya City 2-1.

5 COMMENTS:

  1. Kichuya yupo vizuri ila gemu ya Mbeya city moja katika nafasi alioipata nakujaribu kutoa krosi kwa Boko haikuwa sahihi. Sio dhambi hata kidogo kama kichuya atachukua maamuzi ya kufunga yeye mwenyewe anapokuwa kwenye nafasi. Kichuya ni mfumgaji mzuri tu asisikize maneno ya watu hata wakimuita mroho sawa la msingi ni kufanya maamuzi sahihi.

    ReplyDelete
  2. Goli La Mbeya city kafunga Nani?

    ReplyDelete
  3. Mwandishi sahihisha. Mbeya City ilifungwa 2 ziro

    ReplyDelete
  4. Huyo mwana yanga ya Jangwani

    ReplyDelete
  5. Jaman 2-0 mbona muandishi unatuombea mabaya hatutaki

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic