August 28, 2018



Mshambuliaji nyota Mtanzania, Thomas Ulimwengu anayekipiga nchini Sudan, sasa yuko nchini Misri.

Ulimwengu yuko Misri ambako timu yake ya Al Hilal Omdurman ya Sudan imefunga safari hadi huko kuivaa Al Masry ambayo ilinusurika kung’olewa na Simba katika mechi za Kombe la Shirikisho.

Al Hilal ambao Ulimwengu ni kati ya tegemeo lao, kesho watakuwa na kazi hiyo ngumu dhidi ya Masry na Ulimwengu akiwa kati ya wanaoongoza mashambulizi.

Mechi hiyo itakuwa ni ya Kombe la Shirikisho hatua ya Makundi na Al Hilal imepania kushinda.

Kutoka Port Said nchini Misri, Ulimwengu ameiambia SALEHJEMBE kuwa wamejiandaa vizuri.

"Tumejiandaa vizuri na tunasubiri mechi," alisema Ulimwengu ambaye ni kati ya washambuliaji hatari zaidi raia wa Tanzania wanaochezea nje ya Tanzania.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic