August 29, 2018


Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Mbelgiji Patrick Aussems, amefunguka na kuweka hadharani sababu za kiungo wake, Mohammed Ibrahim kutokupata nafasi.

Tangu msimu wa ligi uanze, kiungo huyo hajapata nafasi ya kucheza kutokana na upana wa kikosi hicho ambao una wachezaji wa kila aina kulingana na usajili ambao imeufanya.

Mbeligiji amesema kikosi cha Simba ni kipana na kina wachezaji walio na ushindani, hivyo hawezi akamuanzisha kama waliopo kwenye kile cha kwanza wanafanya vizuri.

Aussems ameeleza kujituma kwa mchezaji ndiyo kutamfanya apate namba kwenye kikosi chake hivyo kama Ibrahim anataka namba inabidi apambane.

Kocha huyo tangu atue nchini kuanza kibarua na wekundu hao wa Msimbazi, hajapoteza mchezo hata mmoja uwe wa kirafiki au wa kimashindano mpaka sasa.


3 COMMENTS:

  1. Mo Ibrahim yupo sehemu sahihi kama ana malengo ya kweli ya kujiendeleza zaidi kisoka. SIMBA na wanasimba wengi wanafahamu kuwa Mo ni miongoni mwa vijana wa kitanzania wenye vipaji vya hali ya juu na ndio maana Simba hawakuwa tayari hata kidogo kumuacha aende katika dirisha la usajili. Mo anatakiwa lujitunza hasa kiakili kwa kuwa mwingi wa subira huku akimfukuza mwizi kimya kimya kwa kujibidiisha katika mazoezi nafasi itakuja tu ila anatakiwa kujiweka tayari asilimia 100% nafasi itakapokuja amthibitishie kocha kuwa
    alikuwa anakosea kumuweka benchi. Simba inaushindani ila nnaimani wachezaji wanafamu ushindani wao wa ndani ya timu ni kwa ajili ya kuipigania timu kuwa
    miongoni mwa klabu imara zaidi si Tanzania tu bali Africa kwa ujumla kwani mchanganyiko wa wachezaji wa Simba ulivyo wakipewa ushirikiano wa maana basi yajayo kwa Simba yatafuraisha.

    ReplyDelete
  2. Ni kipaji cha levo nyingine kabisa namshauli aache kabisa uvivu afanye mazoezi ya kocha na ajiongeze ya kwake pia ataludi kwenye game insh Allah

    ReplyDelete
  3. Ni mchezaji mzuri na anajituma ndio maana simba wamembakisha, tatizo ni kua namba yake wapo walio zaidi yake !! sasa kusubiri mwenzio ashuke kiwango au limpate balaa la kuumia ndipo wewe ucheze naona jambo hili litashusha kiwango chake ni bora hata kucheza timu ingine kwa mkopo ukiwa na hakika ya kupata namba !!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic