August 29, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema maandalizi baina yao na Rayon Sports kuelekea mechi ya Kmbe la Shirikisho Afrika leo yanaendelea vizuri huko Kigali, Rwanda.

Yanga itashuka dimbani kucheza mchezo wa kukamilisha ratiba na Rayon kutokana na kutokuwa na nafasi tena ya kusonga mbele.

Mratibu wa timu, Hafidh Saleh, amesema wachezaji wote wako vizuri kiafya na hakuna yoyote ambaye yuko majeruhi.

Saleh ameeleza lengo lao kubwa kwenye kipute hicho ni kuweka heshima ya kuhakikisha wanapata matokeo licha ya kuwa hawana nafasi ya kusonga mbele.

Mechi hiyo itaanza majira ya saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki ambapo itachezwa kwenye Uwanja wa Nyamirambo uliopo jijini Kigali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic