August 8, 2018





Yule mwanzilishi wa Sherehe za Simba Day, aliyekuwa mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali amefunguka kuwa siku  hiyo muhimu kwa wanasimba itumike kwa ajili ya kuijenga timu hiyo ili iweze kufanya vyema katika ligi na michuano ya kimataifa kwa kudumisha upendo baina yao pamoja na umoja ili kufanya vyema ikiwa ni pamoja na kuwapongeza viongozi waliopo madarakani akiwemo Mohamed Dewji ‘MO’.

Simba inatarajia kuhitimisha sherehe za Simba Day leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar  kukipiga na Asante Kotoko ya Ghana ikiwa ni mchezo wa kimataifa wa kujipima nguvu ambapo ni sehemu ya  kutambulisha wachezaji wapya wa msimu.

Dalali ikiwa ni kauli mbiu yake katika siku hiyo kwa Wanasimba, ili wawe na msimu mzuri wa ligi kuu, amewataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo  kuendeleza  umoja na mshikamano ndani ya timu ili iweze kuwa nzuri msimu ujao na yenye ushindani wa hali ya juu kwa kuwa wana kikosi kizuri.

“Nashukuru kuona viongozi waliopo madarakani wanaendeleza  tamasha hili la Simba day, mimi nikiwa kama muasisi nawapongeza sana kwani lipo mahususi kwa ajili ya kutuweka pamoja.

“Wanasimba tunatakiwa tuungane tuwe kitu kimoja tuna timu nzuri, tusibaguane tuwe kitu kimoja ili tuweze kufanya vizuri kwenye ligi na hata michuano ya kimataifa,” alisema Dalali.



7 COMMENTS:

  1. Nimeangalia mechi ya Simba na Asante Kotoko. Kiukweli kabisa Simba bado kuna kazi ya kufanya. Kama timu ingekuwa nzuri Simba ingepata goli 3 au zaikai leo. Hata Salamba alipokosa penati, upigaji wa kivivu na wa kishoo . Penati ni nafasi ya kuitumia vizuri. Piga Ukweli bila ushoo hata ukikosa hutajutia. Nawapongeza wachezaji wapya Chama na Hassan Dilunga. Wamedhihirisha wanaweza. Salamba bado sana ushoooshooo mingi. Kocha bado una kazi ya kuwafundisha wachezaji waache ushooooo kuikosesha timu ushindi ni kuwaumiza wapenzi na mashabiki wa timu.

    Reply

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huna lolote nyie kazi yenu kuangalia makosa ambayo kwny mpira yapo,ilhali tumeona hata mchezaji mzoefu Erasto nyoni akifanya makosa!Si mda muafaka kumhukumu salamba bado kijana mdogo anahitaji kujifunza.Istoshe kacheza vzr tu

      Delete
  2. Naona bado muunganiko kitimu hasa fowadi bado haujakaa sawa, mbali na fowadi kushindwa kutumia nafasi chache wanazozipata. Meddy Kagere pia hawajamjulia namna ya kumchezesha, coach wangepitia michezo kadhaa alipokua Gormahia na baadhi ya mechi chache za Kagame cup. Mapungufu mengine ni uharaka (Kuto - delay)kutumia nafasi zinazopatikana,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acheni kulalama bila mpango kocha kakaa na timu wiki mbili lkn ulalamishi tu

      Delete
    2. Jamani mechi ya jana ilikuwa ni Bonanza na sehemu ya kuitambua timu.. Sehemu ya kujifunza makosa yanayowea kutokea kwenye mazingira ya mechi za kimataifa..
      Timu ni nzuri nzuri sana..
      Kuna vitu vichache vya kufanya ili iwe bora zaidi..! Mfano Wachezaji kutokuwa na muunganiko..kutokufahamiana vizuri..mfano Kagere, Okwi.. Wachezaji kama Salamba kucheza na jukwaa hadi akakosa penati..
      Beki ya Wawa na Nyoni kutokuwa na stamina/speed ya mchezo..
      Ni matatizo madogo madogo ya kiufundi..Yakiwekwa sawa timu itakuwa poa sana
      Tatizo la mashabiki maandazi wao wanataka kila mechi washinde tu bila kutaka kujifunza mapungufu yao..!
      Simba is a great team now.. Performance was very good!

      Mimi hofu yangu kubwa ni ubovu wa viwanja vya mikoani.. Na kwa jinsi timu zinavyokamiana ligu kuu lazima majeruhi watakuwa wengi..!

      Delete
  3. Huyu ambae hataki kukosoa timu nenda kaanzishe timu yako maporini huko. Kukosoa ndiokujisahihisha wewe nani utuzuie sisi tusikosoe acha nabiça. Hata kama kocha kakaa na timu siku moja tukiona mchezaji hakucheza vizuri tunasema ili wajitume na wasahihishe mañosa tápate timu bora, wewe Ibrahim nini kinachokukera ? Acha watu waseme fikra zao

    ReplyDelete
  4. hawa watu wanaozuia watu kutoa maoni yao wanakera sana kwa nini tusioe maoni kama tunaona kuna mapungufu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic