Huku ikielezwa kuwa kiungo Haruna Niyonzima ameanza kuzingua ndani ya kikosi cha Simba, uongozi wa timu hiyo umepanga kumpa ufalme kiungo wao mpya, Chama Claytous raia wa Zambia.
Ufalme ambao atapewa Chama ni kama aliopewa Niyonzima msimu uliopita wakati wa Tamasha la Simba Day ambapo Niyonzima alijiungaa na Simba akitokea Yanga.
Katika tamasha hilo la mwaka jana, Niyonzima alikuwa wa mwisho katika utambulisho wa wachezaji huku Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara akisema kuwa kwake mwisho ni kutokana na kumpa heshima fulani ikiwemo utambulisho wa kipekee kuliko wenzake waliotangulia.
Akizungumzia hilo kwa tamasha lao la mwaka huu ambalo linafanyika leo Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na timu hiyo kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana, Manara alisema vile walivyomfanyika Niyonzima mwaka jana, ndivyo watakavyomfanyia Chama mwaka huu.
“Katika Simba Day ya mwaka huu kitu ambacho watu hawapaswi kupitwa nacho ni pale wachezaji watakapokuwa wanatambulishwa kwani itakuwa ni kwa staili ya kipekee.
“Kama mlivyoona mwaka jana Niyonzima tulimtambulisha mchezaji wa mwisho, basi safari hii hilo tutalifanya kwa Chama. Yeye atakuwa mchezaji wa mwisho kutambulishwa na utambulisho wake utakuwa wa kipekee,” alisema Manara.
Huna lolote Manara sifa tu kutegemea fedha za mtu ovyo kabisa
ReplyDeleteNjaa fc acha hasira. Hela za mtu ni zile za Manji, hizi ni za Simba kutokana na uwekezaji kwenye brand kubwa. Hasira peleka Bigwa kwenye matikiti😂😂
DeleteNimeangalia mechi ya Simba na Asante Kotoko. Kiukweli kabisa Simba bado kuna kazi ya kufanya. Kama time ingekuwa nzuri Simba ingepata goli 3 leo. Hata Salamba alipokosa penati, upigaji wa kivivu na wa kishoo . Penati ni nafasi ya kuitumia vizuri. Piga Ukweli bila ushoo hata ukikosa hutajutia. Nawapongeza wachezaji wapya Chama na Hassan Dilunga. Wamedhihirisha wanaweza. Salamba bado sana ushoooshooo mwingi.
ReplyDeleteNimemkubali sana yule Mzambia. Ni fundi haswa. Nilijiuliza kwanini Salamba amepewa nafasi ya kupiga ile penati. Simba inahitaji kuwa na specialists wa penalties, na sio kubahatisha kama ilivyokuwa leo.
ReplyDelete