August 14, 2018


Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema klabu hiyo itaimarika hata zaidi kadiri siku zinavyosonga.

Alisema hiyo hata baada yao kuwazidi nguvu Arsenal mechi yao ya kwanza msimu huu Ligi Kuu England kwa kuwacharaza 2-0 Jumapili.

Gunners walikuwa wanacheza mechi yao ya kwanza ya ushindani bila Arsene Wenger ambaye alikuwa amewaongoza tangu 1996 kabla ya kustaafu mwishoni mwa msimu uliopita.

Lakini hawakujiweza dhidi ya mabinga hao watetezi uwanjani Emirates.

Raheem Sterling aliwaweka City kifua mbele dakika ya 14 na kisha Bernardo Silva akaongeza la pili dakika ya 64.

Upande wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang na nguvu mpya Alexandre Lacazette ndio waliokaribia kufunga lakini bahati haikusimama.

"Tuna wachezaji wengi sana ambao bado hawajafikia kiwango chao cha juu cha uchezaji lakini tumekuwa pamoja kwa misimu miwili na tunajua tunafaa kufanya nini," Guardiola aliiambia BBC Sport baada ya mechi hiyo.

"Tumecheza vyema sana kwa jumla na siku baada ya siku tutaendelea kuimarika na kuimarika.

"Nina furaha kuwa meneja wa Manchester City. Wamenipa kikosi kizuri sana. Siwezi kulalamika hata dakika moja."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic