August 31, 2018


Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, amewataka viongozi wa klabu hiyo kutotetereka juu ya viongozi wake baadhi kuitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Rage amewaomba Simba kuwatetea viongozi hao ambao ni Meneja wa timu, Richard Robert pamoja na Kaimu Katibu Mkuu, Robert Kisiwa baada ya kuitwa TFF kujibu suala la kusababisha wachezaji wa timu yao kuchelewa kuripoti kambini.

Kiongozi huyo amesema Simba wanapaswa kuwaunga mkono kwa kuwapa sapoti ili waweze kuwa washindi akieleza kuwa hakuna kosa lolote ambalo walilifanya.

Rage amewatetea Robert na Kisiwa kutokana na imani yake juu ya taratibu za kuwasili kwa wachezaji ndani ya timu ya taifa kuwa TFF hawatambui vizuri sheria za FIFA.

Mbali na kueleza hayo, Rage pia amesema TFF pamoja na Kocha Emmanuel Amunike, wamewaonea wachezaji hao kwa kuwapa adhabu kubwa na badala yake akashauri vema wangepewa onyo.

3 COMMENTS:

  1. Viongozi wanajiona ni wao tu. Kuna uwezekano timu yetu ya taifa kutetereka kwa kuwakosa wachezaji hao sita na huo utakuwa mwanzo mbaya kwa kocha huyo mpya na pia TFF yenyewe. Busara ndio inayoamuwa matatizo na wala si ubabe. Sio kila anachokitarajia binaadamu kinakuwa miamia, Wakati mwengine hata upepo huipeleka meli kusipopataka. TFF inafaa ijisahihi mapema na wengi wameshapoteza moyo wa kuiunga mkono tifu ya taifa dhidi ya Uganda kwasababu wanapoteza imani kwa siasa hii ya kuangamiza uwezo wa nyota watu kuwafukuza na huku Raisi wetu akiitaka Simba mwaka huu ifanye makubwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Namuona katibu mkuu wa Tff akiwa kama mtu anayepwaya pale

      Delete
  2. Ni lini timu yetu imefanya vizuri kwa kuwa wachezaji nyota? Heri wasio na majina wamewahi kufanya kitu fulani. Nidhamu kwanza, tujifunze kwa waliofanikiwa katika soka.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic