August 31, 2018


Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, amesema kuahirishwa kwa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara zinazohusisha klau za Simba, Yanga na Azam hazitobadili ratiba ya mechi zingine.

Wambura amesema hayo kupitia Radio One, kuwa mechi zingine ambazo zipo kwenye ratiba zitaendelea kama kawaida kama ambavyo imepangwa.

Kiongozi huyo ameeleza Simba, Yanga na Azam wataendelea na vibarua vyao mara baada ya wachezaji wake walioitwa Taifa Stars kurejea.

Wakati Wambura akieleza hayo, tayari wachezaji 6 wa Simba waliokuwa wameitwa kuichezea Stars wameondolewa kutokana na kuchelewa kuripoti kambini.

Hata hivyo TFF na Simba wameitisha kikao na Wanahabari leo kunako makao makuu ya shirikisho hilo ambapo wataweka wazi sakata la wachezaji hao kuondolewa kikosini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic