August 23, 2018


Na George Mganga

Baada ya kushuhudia mtanange wa mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara jana kati ya Coastal Union dhidi ya Lipuli FC, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ametoa onyo kali kwa Waamuzi.

Karia amezungumza hayo baada ya mechi hiyo kumalizika kwa sare ya 1-1 na kueleza kwa msimu huu TFF haitakuwa na msalia mtume kwa Mwamuzi yeoyote atakayeboronga.

Rais huyo amesema kwa sasa hawatakuwa na utani kwani wanahitaji timu kupata matokeo ya halali badala ya kuhusishwa na mlungula ama rushwa jambo ambalo limekuwa likishusha hadhi ya soka la Tanzania.

Baada ya kueleza hayo, Karia amewataka Waamuzi wote kufuata sheria zote 17 za soka kwa kuchezesha bila kufanya upendeleo wowote baada ya pazia la ligi kufunguliwa hiyo jana.

"Waamuzi wanapaswa kufuata sheria na kanuni zote za soka badala ya kulalia upande mmoja, hatutakuwa na huruma kwa yeyote atakayehusika na upangaji wa matokeo kwa msimu huu" alisema Karia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic