August 29, 2018


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya ziara katika Kituo cha Polisi Mabatini ikiwa ni utaratibu aliouweka wa kukakagua jinsi mashauri na mashtaka yanavyoshughulikiwa na askari wa Jeshi la Polisi walioko katika vituo mbalimbali vya jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara hiyo Waziri Lugola amesema amefika kituoni hapo mara baada ya kupokea malalamiko yanayoelekezwa kwa baadhi ya askari wa kituo hicho kutoka kwa wananchi.

Aidha, Lugola, amewazuia askari polisi kutekeleza maagizo ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ya kuwakamata watu na kuwaweka rumande kwa saa 48, ikiwa viongozi hao hawatatoa sababu za kufanya hivyo.

“Maagizo hayo yamekuwa yakitumika vibaya. Kuanzia leo polisi wasikamate mtu yeyote kama DC au RC hajatoa sababu za mtu huyo kukamatwa na ziwe na mashiko. Polisi ukiambiwa kamata mtu bila sababu usimkamate,” amesema Lugola.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic