August 29, 2018


Na George Mganga

Kocha Mkuu wa Simba, Mbeligiji Patrick Aussems, amewataja nyota kadhaa wa timu hiyo ambao wamekuwa kivutio kikubwa kwake tangu aanze kazi rasmi na klabu hiyo kongwe hapa nchini.

Kwa mujibu wa Magic FM, Aussems amesema amekuwa akifurahishwa zaidi na kiwango cha starika aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia FC, Meddie Kagere akimuelezea kama mtu shupavu ambaye anapambana akiwa na mpira.

Aidha, Aussems amewataja wachezaji kama John Rafael Bocco licha ya kuwa na majeruhi ya muda mrefu lakini anaamini kiwango chake na namna anavyojituma kwenye mazoezi kinamshawishi kumpa nafasi ya kucheza.

Mbali na Bocco, Aussems amewataja pia wachezaji Emmanuel Okwi, Adam Salamba kuwa na kiwang kizuri Uwanjani kwa namna ambavyo wamekuwa wakionesha jitihada mazoezini na kwenye mechi.

Ukiachana na waliotajwa hapo juu Aussems amesema kwa ujumla wachezaji wote wa Simba wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya timu na amekuwa anapata ushirikiano mzuri tangu aanze kuwanoa.

Wakati akifunguka hayo, Aussems hivi sasa yupo katika maandalizi ya kukinoa kikosi cha Simba kuelekea mechi zijazo za ligi ambapo walipaswa kucheza na Lipuli FC Septemba Mosi 2018 japo mechi hiyo imehairishwa baada ya wachezaji wake wengi kuitwa Taifa Stars.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic