SABABU ZA BOCCO KUZIKOSA MECHI MBILI ZA KIRAFIKI UTURUKI
Kutokana na kuendelea kukoseakana katika kikosi cha Simba kilichocheza mechi za kirafiki huko Uturuki, inaelezwa kuwa Nahodha wa timu hiyo, John Bocco, bado hajawa fiti.
Taarifa kutoka Instabul katika milima ya Kartepe huko Uturuki ambapo Simba imepiga kambi ya wiki mbili, zinasema Bocco bado hajapona vizuri kitu kilichopelekea akose mechi hizo.
Mpaka sasa Simba imeshacheza mechi mbili dhidi ya Mouolodia FC ya Morocco ambayo walitoka nayo sare ya 1-1 huku jana ikicheza pia na Ksaifa ya Palestina na kushinda mabao 3-0.
Katika mechi hizo zote, Bocco hajacheza hata moja kutokana na majeruhi yake kuendelea kumpa wakati mgumu ambapo bado hajapomna.
Baada ya jana kukipiga dhidi ya Ksaifa, Simba inatarajiwa kuanza safari leo ya kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya tamasha lake la Simba Day litakalopigwa Agosti 8.
0 COMMENTS:
Post a Comment