UONGOZI YANGA WATOA RIPOTI YA MICHANGO YA FEDHA
Na George Mganga
Uongozi wa Yanga umesema maendelo ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuisaidia klabu hiyo unaendelea vizuri.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya klabu hiyo kutangaza rasmi juzi Ijumaa utaratibu mzima wa kuichangia kwa kutoa namba maalum zitakazowawezesha wadau wake kutuma fedha.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari Msaidizi, Godlisten Anderson kupitia Radio One, alisema wanayanga wameanza kwa kasi nzuri huku akiomba wazidi kuendelea kuchanga ili hamasa iwe kubwa.
Hatua ya Yanga kuomba michango imekuja kutokana na klabu kupitia kipindi cha mpito hivi sasa, jambo ambalo limepelekea iweze kuyumba kiuchumi.
Wakati wanachama, mashabiki na wadau wa Yanga wakiendelea kuichangia klabu yao, kikosi cha klabu hiyo kipo Morogoro hivi kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.
Yanga imeweka kambi ya wiki mbili kwa ajili ya kuwawinda waarabu hao Agosti 19 2018, ikumbukwe katika mechi ya awali, Alger walishinda mabao 4-0 wakiwa kwao.
Mbona Husemi Kama tumeshachanga shilingi ngapi mpaka sasa ili Tupate mzuka
ReplyDeleteHawasemi kwasababu hiyo ni siri la muhimu ni tuzidi kujitutumua. Ningeshauri vilevile wachezaji na kikosi cha ufundi nao pia wawe tsyari kuchanhia kitu kila mwezi ili mahasimu wetu watahayari waondoke na dhana kuwa yanga itachechemea na jinsi mapendo yetu yalivo
ReplyDeleteMimi sijaona namba za kuchangia.
ReplyDeleteMbona hakuna ripot mwandishi acha kuchapa uongo
ReplyDeletehuu usanii hadi lini? pengine nyie wanahabari hizi habari so za kweli!
ReplyDelete