August 27, 2018




Akitokea benchi, Mbwana Samatta ameendelea kucheka na nyavu akiwa na KRC Genk baada ya kuisaidia kushinda kwa mabao 3-2 dhidi ya Waasland Beveren.

Bao hilo linamfanya nahodha huyo wa Taifa Stars afikishe mabao nane katika mechi tano ambazo amefunga mfululizo kila alipoweka miguu yake uwanjani.

Samatta aliingia katika dakika ya 59 na dakika ya 78 akaisawazishia Genk bao baada ya Beveren kufunga bao la pili katika dakika ya 66.

Ushindi wa Genk ulipatikana dakika ya 89 baada ya beki wa Beveren kujifunga wakati akijaribu kuokoa.

Samatta amekuwa na mwendo mzuri wa kupachika mabao mfululizo katika kikosi cha KRC Genk.

Wiki iliyopita, Samatta alifunga mabao matatu wakati Genk ikiichapa Bondby katika Play off za Europa League kwa mabao 5-2.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic