Na George Mganga
Kikosi cha wekundu wa Msimbazi, Simba, kimewasili salama jijini Arusha baada ya kuitikia wito wa Mkuu wa Mkoa huo, Mrisho Gambo.
Simba wametua majira ya usiku wa jana wakitokea Dar es Salaam ambapo kikosi chake kinatarajiwa kucheza mchezo mmoja wa kirafiki kuelekea mechi ya Ngao ya Hisani.
Gambo amewaalika Simba kwa ajili ya kucheza na Arusha United ambayo ilikuwa inajuliakana kama JKT Oljoro iliyopo Ligi Daraja la Kwanza.
Simba watacheza na Arusha United kesho Jumatano ambapo leo kikosi kitapumzika kwa ajili ya kujiandaa na mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini humo.
Kikosi cha Simba kitautumia mchezo huo kama maandalizi kuelekea mechi dhidi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Sugar itakayopigwa Agosti 18 kwenye Uwanja wa CCm Kirumba, Mwanza.
SIMBA nguvu moja wachawi na wenye roho ya husda watateseka sana mwaka huu.
ReplyDelete