August 14, 2018


Uongozi wa klabu ya Simba umefichua siri ya kushindwa kuwafunga Namungo FC ya Ruangwa, Lindi baada ya kwenda nayo suluhu ya 0-0.

Simba walikuwa na mchezo wa kirafiki siku mbili zilizopita dhidi ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza kwa ajili ya uzinduzi wa Uwanja wa Majaliwa uliopo mjini Ruangwa.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari Simba, Haji Manara, amesema waliamua kutowafunga Namungo ili kuweka heshima kutokana mwaliko wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Majaliwa aliwaalika Simba ili wakacheze na Namungo kwa ajili ya uzinduzi hivyo Manara ameeleza ilibidi watumie busasara ili wasiweze kuleta aibu kwa Waziri.

"Tuliamua kutowafunga Namungo kwa ajili ya heshima ya Waziri, hauwezi kumwaibisha mtu mkubwa kama yule mwenye heshima zake" alisema.

13 COMMENTS:

  1. Tatizo tuna pesa lakini tumesajili wachezaji wazee. Mi huwa sielewi kwa nini inakuwa hivyo. Angalia Erasto Nyoni,Okwi,Wawa,Kagere,Bocco,Niyonzima, Dida na wengine wengi waliodanganya umri. Sijui hata hiyo mechi ya kirafiki na Timu ya Arusha kama tutashinda. Na kuna uwezekano Mtibwa ikatufunga japokuwa imefungwa mechi zake zote za pre -season. Hatujashinda hata mechi moja ukiacha ile wapinzani wanayosema tulicheza na madereva teksi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. MMM WEWE MWENZETU KWELI? HUELEKEI KUWA SIMBA. KWA TAARIFA HAO WAZEE NDIO UZOEFU WAO TUNAUTAKA WAKIUNGANISHA NA KINA DILUNGA, GYAN, MLIPILI, CHAMA, KICHUYA, MBONA TIMU NZURI TU. LAKINI UNAPOSEMA WAMEDANGANYA UMRI SIO BUSARA UNAWAKOSEA HESHIMA BINADAMU WENZIO. WAHESHIMU TU MBONA WEWE HAKUNA ANAYEHANGAIKA KUJUA UMRI WAKO?

      Delete
    2. Acha upambe wewe fala.Usijisingizie vitu vya hatari(Simba).. wazee wamezaa na bibi yako.???

      Delete
    3. Achana na simbs yetu ya wazee, tafuta timu yako ya vijana uende huko.

      Delete
    4. TATIZO NDUGU ZANGU TEELEWE KUA SIMBA IPO KATIKA MAZOEZI KUSHINDA SI ISSUE SANAKWANI MUHIMU KUANGALIA MAPUNGUFU NA KUYAFANYIA KAZI.KUHUSU WACHEZAJI HAKUNA MZEE KWANI KAMA ANAKITUNZA NA KUFAHAMU MAJUKUM YAKE AKIWA UWAJNANI SI ISSUE KWANI YTUMESHUDIA VIJANA WADOGO UNAHOWAFAHAM WEWE MPIRA UMEWASHINDA.NYONI HANA MUDA GANI ANACHEZA???NAFIKILI TUSPENDE SANA MATOKEO TUKAJA KUTAFUTANA BAADAE KWANI LINGI NDIO MCHEZO WA USHINDANI NA SIVINGINE.

      Delete
  2. INGEPENDEZA KUSEMA - NAMUNGO NI TIMU NZURI YENYE WACHEZAJI MAHIRI WALIOCHEZA KWA KIWANGO CHA JUU NA KUWEZA KUTOKA SARE NA SIMBA, TUNAWAPONGEZA -.

    ReplyDelete
  3. Eti Emma Okwi mzee! Wewe vipi? Hao wengine wote uliowataja tunawaita experienced players, na sio wazee. Wangekuwa wazee kama unavyodai Bocco na Nyoni wasingekuwa wachezaji bora wa VPL msimu uliopita. Okwi pia asingekuwa mfungaji bora. Huyo Kagere kwa sasa ndiye foward anayeogopwa zaidi Afrika Mashariki. Subiri ligi ianze ndio utawajua vizuri hao watu na utaona aibu kwa kauli yako hii ya kipuuzi kuhusu hayo majembe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ww Manara na simba kwa ujumla msituletee mambo ya kijinga kwenye soka eti mliamua musiwafunge mkatoa sare kwa ajili ya heshima ya waziri Mkuu kwanini musiamue kufungwa na Namungo ili heshima iwe juu zaidi kwa Mheshimiwa? Wacheni longolongo mpira uwanjani nyinyi c anacheza kwenye media.........

      Delete
  4. Ikiwa Bwana kulialia HSM kaanza kwa kusema maneno ya aina hii tutarajie shutma kubwa kwa marefa na viwanja msimu huu.

    ReplyDelete
  5. Inachekesha pale mnazi wa Yanga huku akijifanya Simba anapojifanya kutoa maoni ya kuwaponda wachezaji wa Simba kuwa ni wazee? Kwa taarifa tu hakuna mchezaji mzee pale Simba. Wachezaji wengi wa Simba wanamiaka kadhaa mbele ya kusakata soka na bado wakawa Lulu kama si dhahabu. Hao wanaodaiwa kuwa ni wazee pale Simba kama wangeamua kuchukua majukumu ya kinda na kijana Salamba siku ya mechi ya Kotoko kwenda kupiga penalt basi leo tungekuwa tunazungumzia lugha nyengine. Kwani jina la muhenga la Okwi limekufia wapi? Sport pesa kule kenya kikosi kinda cha simba kiliteseka hadi shida na kukosa nafasi yakwenda kujitangaza zaidi Uingereza na watu wakalani na kuhoji kwanini Okwi, Boko hawakujumuishwa kwenye msafara wa kenya? Hao wanawaita wachezaji wazee Simba ni mastaa wa kweli sio mchezo na ngoja ligi ianze. kilichobakia ni wivu tu na kuwatupia maneno ya kijinga na kejeli za kichawai.

    ReplyDelete
  6. Manara always under overstastement in fact huna lugha ya mpira inayosema kuachiana mbona hawajajifunga wenye ili heshima iwe juu zaidi kwa waziri mkuu alafu siku zote chakwako lazima ukipambe

    ReplyDelete
  7. Bongo mbaya hadi leo Christiano Ronaldo hajaitwa Mzee na miaka yake 33!! Ila hawa wa kwetu wa miaka 30 hadi 32 ni mababu! Ndo maana akina Babi, Chuji, Kavila na Kaseja hawazitaki timu zenu hizo!!

    ReplyDelete
  8. Jamaa anasema kweli. Hao wachezaji ni wazee kuliko mdhamini wa timu. Huwezi linganisha umri wa Kagere au Wawa na Mo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic