August 28, 2018


Uongozi wa klabu ya Lipuli FC ya Iringa pamoja na Simba umekubaliana kucheza mechi ya Ligi Kuu Bara kama ambavyo ilikuwa imepangwa kupigwa Septemba Mosi 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, imeelezwa.

Timu hizo zianeleza kufikiwa kwa mwafaka huo na kuamua kuliandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zikiomba mechi hiyo ichezwe tarehe hiyo baada ya kutangazwa kuahirishwa kutokana na wachezaji 7 wa Simba kuitwa Taifa Stars.

TFF kupitia Bodi ya Ligi iliamua kuahirisha michezo inayihusisha timu tatu ikiwemo Yanga na Azam baada ya wachezaji wake wengi kuitwa kwenye timu ya taifa ambayo inaingia kambini Agosti 30 kuanza maandalizi ya kucheza na Uganda kwa ajili ya kufuzu AFCON.

Simba wameamua kuigunga mkono Lipuli ambayo tayari ilikuwa imeshaweka kambi jijini Dar es Salaam, kutokana na kuwa na kikosi kipana ili kuipunguzia gharama za usafiri na malazi.

Kuelekea mechi hiyo, timu zote mbili zinaendelea kujifua tayari kwa mechi hiyo ambayo itaamuliwa na Bodi ya Ligi kama itachezwa tarehe ambayo pande zote mbili zimekubaliana kipute kipigwe.

2 COMMENTS:

  1. Kukosekana kwa Wadhamini kwenye ligi kuu msimu huu tutaonana mengi. Timu ndogo haziwezi tena kutoa ushindani kama ilivyokuwa miaka miwili mitatu nyuma. Itafikia kipindi hizi timu zitashidwa kusafiri na zitasafirishwa na timu zenye pesa. Hakuna tena ligi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic