August 28, 2018


Baada ya straika hatari, Meddie Kagere 'MK 14' kutupia mbili kambani na kuipa Simba ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City jana, mashabiki wa Yanga walijikuta kwenye wakati mgumu taifa jana.

Mashabiki hao baadhi walijitokeza jukwaani kusini magharibi kwa Uwanja kama ilivyo kawaida yao wakiwa na jezi za njano, walijikuta wakianza kuondoka taratibu baada ya mambo kuanza kugeuka.

Kuondoka kwa mashabiki hao kulisababisha na balaa la Kagere ambaye alianza kucheza na nyavu mnamo dakika ya 12 kipindi cha kwanza na baadaye kuelekea mwishoni mwa kipindi cha kwanza akapachika la pili.

Wakati mashabiki hao wakiwa Uwanjani, mapema baada ya mechi kuanza walikuwa wanaipa sapoti ya nguvu Mbeya City, lakini mambo yakaenda sivyo na kila mmoja akaanza kuelekea njia yake nje ya Uwanja.

Kagere sasa amefikisha mabao matatu ambayo amefunga ndani ya mechi mbili ikiwa ni pamoja na lile moja alilowalaza Tanzania Prisons kwenye mechi ya ufunguzi.

Baada ya Simba kumalizana na Mbeya City jana, mchezo utakaofuata itakuwa inacheza dhidi ya Lupuli FC ya Iringa.

4 COMMENTS:

  1. Mbeya City haina jipya imebaki jina tu! Hatushangai kufungwa kwao kila mmoja alitarajia hilo!

    ReplyDelete
  2. Mbeya city haina jipya ila Kagere ni hatari. Yanga na mashabiki wake ni watu kuchonga sana na kama kagere angekuwa mchezaji wa Yanga basi SIMBA na mashabiki wake wangeteseka sana na maneno ya kejeli. Kuna wanazi wa Yanga waliolewa ushabiki tayari walishasema kwa makambo wa Yanga washambuliaji Simba watapata taabu sana. Kweli? Wanamuelewa Meddy Kagere vizuri lakini? Kagere ni mshambuliaji msumbufu na nguvu yaani Diego Costa wa East Africa.

    ReplyDelete
  3. Yanga walibahatisha tu mechi ya waarabu na mtibwa..hata wakicheza na mbeya city leo hawatapata takwimu ya ball possesion ya asilimia 70.sawa wao wataendelea na bahati zao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic