August 29, 2018


Yanga wamelalamika kusota jana Uwanja wa ndege wa Kigali kwa dakika 40, lakini kwa mujibu wa mchambuzi wa soka wa Rwanda, Clavour Kazungu si Shirikisho wala klabu waliokuwa na taarifa.

Yanga ilitua Jumanne alfajiri tayari kwa mechi ya leo saa 10 jioni dhidi ya Rayon kwenye Uwanja wa Nyamirambo am­bayo ni ya kukamilisha ratiba ya michuano hiyo ingawa wenyeji wakishinda wanapindua meza.

Mchezo huo unatarajiwa kucheza leo Jumatano saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Nyami­rambo, ambao kama Wanyar­wanda hao wakishinda basi wana nafasi kubwa ya kufuzu kwenda robo fainali ya kombe hilo.


Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema kuwa timu hiyo ilifika kwenye Uwanja wa Ndege huo saa 12:00, asubuhi na kukalishwa hapo hadi saa 12:40, wakisubiria wenyeji wao.

Saleh alisema, hawashangai kwa hicho kilichotokea kwani ni kawaida kutokea katika michuano hiyo kwa wenyeji kufanya maku­sudi, hivyo hali hiyo haiwasababishi wao kutoka mchezoni zaidi wanaji­panga kwa ajili ya mechi hiyo.

“Jambo la kwanza kabisa ni kush­ukuru kuwa tumefika salama, lakini hayo mengine yanakuja baadaye ya kuwekwa uwanja wa ndege kwa dakika 40 na wenyeji wetu.

“Hayo ni masuala ya kifitna ambayo hutokea na mara ny­ingi tumekutana nayo kutokana na uzoefu wetu wa ushiriki mi­chuano ya kimataifa ikiwemo hiyo ya kuwekwa uwanja wa ndege kwa makusudi,”alisema Saleh.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic