August 29, 2018


Na George Mganga

Yanga imekamilisha ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kufungwa bao 1-0 na Rayon Sports katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Nyamirambo, Kigali, Rwanda jioni ya leo.

Bao pekee la Rayon limewekwa kimiani na Bimenyimana mnamo dakika ya 19 kipindi cha pili na kuhitimisha dakika zote 90 matokeo yakiwa hivyo.

Licha ya Rayon kupata matokeo, Yanga walionekana kutawala zaidi mchezo kwa dakika zote 90 lakini mapungufu kadhaa haswa katika safu ya ushambuliaji ya yamechangia kushindwa kucheka na nyavu kutokana na kupata nafasi nyingi za kufunga.

Mechi hiyo imechezeka huku mvua ikinyesha haswa kipindi cha kwanza na kupelekea maji kiasi kutuama ndani ya nyasi za Uwanja wa Nyamirambo na kuleta ugumu wa mpira kutambaa vizuri.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga imalize mechi zake ikiwa nafasi ya nne mkiani na pointi zake 4 huku Rayon wakishika nafasi ya pili kwa kuwa na alama 9 baada ya kuishusha Gor Mahia ambayo imefungwa na USM Alger kwa mabao 2-1 leo.

USM Alger imejiongezea alama tatu leo baada ya kuwalaza Gor Mahia ambao wana pointi 8 pekee na kufikisha 11. 

4 COMMENTS:

  1. taharifa za yanga zinaandikwaga kipoleeee....kwanini msiandike kikosi cha mauwaji cha kalia kidude au Makombo kama siyo makambako achemsha kwa wanyarwanda...

    ReplyDelete
  2. Nilishagundua waandishi hapa wanaegemea Yanga na habari za Yanga wanazirembesha sana!

    ReplyDelete
  3. Andika kwenye kichwa cha habari kuwa Yanga wamefungwa! Sio wametimiza ratiba!

    ReplyDelete
  4. Vipi Makambo hakucheza leo? Au ndio hivyo tena kachemsha na mapema yote hii?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic