September 23, 2018





Na Saleh Ally, Polokwane
Mtanzania Abdi Banda, ameteuliwa kuwa nahodha wa kikosi cha Baroka FC kinachoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Kutokana na kupata nafasi hiyo, Banda aliyewahi kuzichezea Coastal Union na Simba anakuwa Mtanzania wa kwanza kupata nafasi ya kuwa nahodha wa timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Banda ametangazwa kuwa nahodha wa timu hiyo inayotokea katika mji huu wa Polokwane ikiwa mara ya pili akivaa kitambaa cha unahodha.

Banda alianza kuvaa kitambaa hicho katika mechi iliyopita, lakini leo tena wakati Baroka ikiivaa Orlando Pirates na kupoteza kwa mabao 2-1, Kocha Wedson Nyirenda kutoka Zambia alimpa nafasi hiyokwa mara ya pili.

Wakati akimpa kitambaa hicho baada ya nahodha kupumzishwa, Banda alikabidhiwa kitambaa hicho na kuiongoza Baroka FC hadi mwisho wa dakika 90.

Orlando ilitawala katika kipindi cha kwanza na kupata mabao mawili huku Baroka FC wakitawala kipindi cha pili katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Peter Mokaba jijini Polokwane na Banda aking'ara zaidi.

1 COMMENTS:

  1. Wachezaji wengine hebu igeni kwa banda msiridhike tu simba na yanga tu nidhamu ndiyo nguzo yenu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic