September 23, 2018


Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amesema wanaotumia ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kama mtaji wa kisiasa watakamatwa na kuchukuliwa hatua.

Lugola ametoa kauli hiyo alipowasili katika eneo la tukio kilipozama kivuko hicho huko Ukara Ukerewe mkoani Mwanza akitokea Kigoma ambapo amesitisha ziara yake ya kikazi na kulazimika kuelekea Jijini mwanza kufuatilia ajali ya MV Nyerere.

“Hatuko tayari kuchonganisha serikali na wananchi wake kupitia tukio hili. Tutakaowabaini tutawakamata.”

Lugola amesema zoezi la uokoaji na uopoaji litaendelea mpaka hatua ya kivuko kuondolewa majini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic