September 25, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuanza kutupiwa kejeli kutoka kwa watani zake wa jadi ikiwa ni siku mbili tangu aeleze kuwa anasumbuliwa na tumbo, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema kwake ni jambo la kawaida.

Manara alishikwa na homa ya tumbo wakati akiwa jijini Mwanza kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Mbao na kupelekwa hospitalini kwa ajili ya vipimo zaidi kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam jana jioni.

Kutokana na kushikwa na tumbo hilo, baadhi ya mashabiki wa Yanga walianza kumtania kuwa yawezekana kichapo walichokipata Simba cha bao 1-0 dhidi ya Mbao kimesababisha tumbo hilo limuume.

Aidha, wapo wengine waliomtania kuwa tayari ameshaanza kushikwa na kiwewe kuelekea pambano la watani wa jadi dhidi ya Yanga litakalopigwa Septemba 30 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Licha ya kutaniwa Manara amesema si kipigo cha Mbao wala Yanga ambao wamesababisha ashikwe na tumbo hilo bali ni majaaliwa ya Mwenyezi MUNGU.

"Ni tumbo pekee lilikuwa linasumbua na tayari nimehafanyiwa vipimo, nimeshikwa nalo sababu ya majaaliwa ya Mwenyezi MUNGU, si kweli kuwa Mbao au Yanga wamesababisha niwe kwenye hali hii" alisema Manara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic