September 25, 2018


Na George Mganga

Ikiwa ni wiki ya moto kuelekea pambano la watani wa jadi Jumapili ya Septemba 30 2018, kikosi cha Yanga kimeondoka jana jioni kuelekea mjini Morogoro kuweka kambi maalum kujiandaa dhidi ya Simba.

Yanga wameondoka Dar es Salaam kwa ajili ya kambi hiyo ili kujiweka fiti tayari kusaka mbinu za kuchukua pointi tatu ili kuzidi kujiweka kileleni.

Uongozi wa klabu hiyo umeamua kuipelekea timu Morogoro kutokana na namna mechi hiyo ilivyo na msisimko wa aina yake ili kuwapa wachezaji wake utulivu mzuri kabla ya kucheza na Simba.

Aidha, Yanga wamekipeleka kikosi Morogoro wakiamini ni sehemu tulivu ambayo itawapa wachezaji nafasi nzuri ya kutopata bughdha tofauti na ilivyo Dar es Salaam jiji ambalo lina pilikapilika zisizoisha.

Mchezo huo wa watani wa jadi utakuwa wa kwanza kwa msimu huu huku ukisubiriwa kwa hamu kubwa na wadau pamoja na mashabiki wa soka la Tanzania kutokana na timu zote kuonesha dhamira ya kuutaka ubingwa wa ligi msimu huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic