September 26, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuelezwa kufungiwa na Shirikisho la Soka Duniani kwa muda wa miaka miwili, imeripotiwa kuwa kiungo wa Yanga, Mohammed Issa Banka, amezua tafrani katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia Spoti Leo, kilieleza kuwa Banka amezua tafrani katika baraza hilo ambapo mpaka sasa halijapata taarifa rasmi kutoka Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) juu ya sababu rasmi za kusimamishwa kucheza soka kwa mchezaji huyo.

Baraza hilo limeshangazwa na ZFA kutokutoa taarifa rasmi mpaka sasa juu ya Banka ambaye ameelezwa kufungiwa miaka miwili na FIFA kwa kutuhumiwa kutumia sigara bwege 'Bangi'.

Mpaka sasa Banka ameendelea kujifua mchangani visiwani humo baada ya kifungo hicho huku ndoto zake za kucheza soka Yanga zikiwa zimelala kwa kipindi hiki.

Mchezaji huyo alisajiliwa Yanga kwa muda wa miaka miwili akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro ambayo ilikuwa haijamtumia kwa muda baada ya maafikiano na Yanga kufikia mwafaka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic