September 26, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Singida United umeamua kuvunja ukimya kuhusiana na hali yao namna ilivyoyumna kiuchumi kipindi hiki tangu kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

Singida wameeleza kukiri kuwa klabu yao kwa sasa inapitia hali tete kutokana na baadhi ya wadhamini walionao kuondoka ikiwa ni pamoja na kutokupatikana kwa mdhamini wa Ligi Kuu.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka Singida United zinasema hali waliyoanza nayo awali si kama ya sasa jambo ambalo limepelekea hata baadhi ya wachezaji kuanza kujiengua kutokana na madai ya stahiki zao.

Hivi karibuni kipa wa timu hiyo, Manyika Peter aliondoka ndani ya klabu hiyo akidai kutolipwa fedha zake za usajili pamoja na fedha za mshahara wa miezi kadhaa.

Aidha, makocha wasaidizi Jummane Challe na Athuman Mfaume nao walijiengua kwa suala lilelile la kudai fedha zao ambapo imeelezwa nafasi zao zimechukuliwa na Nizar Khalfan.

Ukiachana na wasaidizi, ilielezwa pia kuwa kiungo wake Mganda, Shafik Batambuze ameshaanza kufanya mazungumzo na Gor Mahia ili wamsajili kutokana na stahiki zake ndani ya Singida kutotimiziwa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic