September 6, 2018


Mshambuliaji wa klabu ya Simba Meddie Kagere amemtisha nyota wa zamani wa Yanga, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ ambaye anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja katika ligi Kuu Tanzania Bara akiwa amefunga mabao 26.

Hadi sasa Kagere ndiye kinara wa ufungaji kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara akiwa tayari ameshafunga mabao matatu kwenye michezo miwili ambayo alishuka uwanjani mbele ya Tanzania Prisons na Mbeya City.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mmachinga amesema Kagere anaweza kuifikia na kuivunja rekodi yake ya kufunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja aliy­oweka mwaka 1999 aki­itumika Yanga, ikiwa ni takribani miaka zaidi ya 18 imepita toka aweke rekodi hiyo.

Mmachinga ambaye ali­wahi pia kukipiga Simba mwaka 2000 na kutwaa ubingwa wa Safari Lager (sasa Ligi Kuu) mwaka 2001 ambapo mwaka huo huo alistaafu kucheza soka.

“Kagere akiongeza juhudi kidogo anaweza kuifika rekodi yangu kwa sababu jamaa ana nguvu, anaweza kufunga mabao kwa staili zote lakini kubwa kabisa ana juhudi za kutafuta mabao.

“Hivyo namuona kabisa aki­itishia rekodi yangu ya kufunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja ambayo ni 26 kama akiongeza juhudi,” alisema Mmachinga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic