September 5, 2018


Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu Omary Kaya, umesema hautazungumzia lolote juu ya suala la mchezaji wao Mohamed Issa Banka kufungiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

Kaya ameeleza kuwa hawatasema lolote bali watasubili kauli husika kutoka kwa shirikisho la soka Tanzania (TFF) kuwapa ukweli kuhusu suala hilo kama amefungiwa au sivyo.

Taarifa zilizotoka jana zinaeleza kuwa Banka amefungiwa na CAF kwa miaka miwili baada ya kufeli vipimo walivyochukuliwa kwenye michuano ya Cecafa Challenge Cup iliyofanyika Kenya November 2017.

"Sisi kama uongozi wa Yanga hatuwezi kusema chochote kuhusiana na mchezaji Banka, tunasubiri taarifa kutoka TFF na baada ya hapo tutaweza kuzungumza ya kwetu" alisema.

4 COMMENTS:

  1. Yanga wameingizwa mkenge na Mtibwa. Lakushangaza Viongozi wa Yanga wanajizonga wenyewe na kauli zao zisizoeleka. Jana tu iliripotiwa kuwa kuwa viongozi wa yanga walikuwa wanafahamu kuwa mchzaji huyo kafungiwa na CAF ila wamemsajili kwa baadae. Baadae miaka miwili? Kama si uzimwamwa kitu gani? Leo hii viongozi hao hao wanasema kuwa hawana uhakika kama mchezaji huyo kafungiwa na CAF au La? Kwa kweli ni ubabaishaji wa hali ya hovyo kabisa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Baadae hujui SKAUTING ? Tunasajili kwa kuangalia mbali sana. Inaitwa SKAUTING.

      Delete
    2. Vyombo vingi vya habari ni vyombo vilivyopo kwa ajili ya kutengeneza pesa na si kutoa taarifa sahihi. Taarifa nyingi hazina uchunguzi wa kutosheleza ndio maana zinaishia juu juu. Yanga hawajatoa tamko la Banka kama kafungiwa au la..yote yanayosemwa ni vyombo vyetu vya habari ndio vinatoa hizo kauli. Kama ni kweli Banka kafungiwa au la..hiyo itakuja kutolewa taarifa zake muda si mrefu. Sidhani kama viongozi wa CECAFA wangekaa kimya baada ya hivyo vipimo. Lazima tungejua kuna mchezaji kakamatwa wakati wa vipimo. Washabiki na wapenzi wa Yanga wawe watulivu taarifa itatoka muda si mrefu kuhusu hilo

      Delete
    3. Heheheeee...yetu macho na masikio

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic