September 5, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa Yanga umetangaza kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya African Lyon Jumapili ya Septemba 9 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga watakipiga na Lyon ambapo mechi hiyo itaanza majira ya saa 10 kamili jioni huku mchezo huo ukienda mbashara kupitia Azam T.

Kuelekea mechi hiyo, viingilio vya mchezo vitakuwa ni 3000 kwa mzunguko, 5000 kwa VIP B na 10000 kwa VIPA A.

Yanga imeamua kucheza na Lyon baada ya ule mpango wa kusafiri kuelekea Kigoma wakacheze na Singida United kuahirishwa kutokana na Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera, kutaka wachezaji wake wapumzike.

Wakati huohuo watani zao wa jadi Simba, nao watakuwa Uwanjani hapo Jumamosi ya wiki hii kucheza mechi ya kirafiki na AFC leopards ya Kenya majira ya saa 1 jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic