September 23, 2018




Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefichua kwamba mshambuliaji wa timu hiyo, Mrundi, Amissi Tambwe anatakiwa apunguze kilo tano ili aweze kwenda sawa na kasi yake lakini imekuwa ngumu kutokana na kupenda kula ugali.

Zahera mwenye uraia wa DR Congo na Ufaransa, ameyasema hayo kufuatia mfungaji bora huyo wa zamani katika msimu wa 2013-14- na  2014-15 kushindwa kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union uliopigwa juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa ambao Yanga ilishinda bao 1-0.

Zahera alisema  kuwa amekuwa akizungumza na mshambuliaji huyo mara kwa mara juu ya suala la kutakiwa kupunguza kilo hizo lakini inaonekana amekuwa mbishi kutokana na kupenda kula ugali.


“Tatizo kwanza amekuwa mwoga kwa sababu alikuwa kwenye majeraha na ndiyo yamesababisha ashindwe kucheza vile inavyotakiwa kutokana na uwezo wa kawaida alioonyesha kwenye mchezo wa leo (juzi) hakuwa na kipya cha kushangaza.


“Unajua nimekuwa nikimwambia apunguze uzito kwa kuondoa kilo tano lakini naona amekuwa mbishi hataki kufanya hivyo kwa sababu anapenda kula ugali sana matokeo yake hafuati kile ambacho anatakiwa kufanya,” alisema Zahera.

1 COMMENTS:

  1. Makocha wa hizi timu sijui wametoka wapi?Kocha amejua tatizo anasema hadharani eti amekuwa mbishi anapenda ugali!!!Wewe kocha kazi yako nini?Kama mchezaji hataki kufuata maagizo wa nini kwenye timu?Inashangaza sana. Waandishi uchwara nao hawaulizi maswali.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic