September 23, 2018





Kocha wa timu ya Stand United, Amas Niyingabo, baada ya mshambuliaji wake ambaye aligeuka mwiba kwa Yanga, Alex Kitenge kufunga ‘hat-trick’ ameibuka na kusema kuwa kwa jinsi anavyoona uwezo wa mchezaji huyo, ataweza kufunga mabao zaidi ya 20 kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu.


Kitenge alikuwa mwiba kwenye mechi dhidi ya Yanga iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa kwa kufunga mabao matatu.


Niyongabo alisema kuwa anamjua mshambuliaji wake ni mchezaji mwenye uchu wa kufunga hata kwenye mechi za nyuma aliweza kugongesha mwamba mara tatu, hivyo msimu huu anaamini anaweza kufunga mabao zaidi ya 20.

“Kitenge msimu huu atafunga mabao mengi sana kwani nilimuangalia katika mechi za nyuma alizocheza lakini mashuti yote aligongesha mwamba kwani ni mtu mwenye uchu wa kufunga muda wote, msimu huu ataweza kufikisha mabao 20 na kitu hivi,” alisema Niyongabo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic