September 3, 2018


Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa makini na Waamuzi wa ligi.

Rage amesema hayo kutokana na baadhi yao kuanza vibaya kwa kutoa maamuzi ambayo hayastahili katika mechi za mwanzo za Ligi Kuu Bara.

Kiongozi huyo wa zamani wa Simba amewataka TFF kujaribu kuwaangalia kwa umakini waamuzi hao ili wasije wakaleta shida katika soka letu ikiwemo kuwapa somo la sheria 17 za mchezo wa soka.

Rage amefunguka hayo kutokana na mwanzo huo kuwa mbaya kwao akiamini wanaweza kuleta taswira mbovu kwa wadau wa michezo na kuharibu ladha ya mpira wa miguu nchini.

Katika mechi za mwanzo ikiwemo ya Coastal Union dhidi ya Biashara kuleta utata wa bao la mpira wa FREE KIKI kwa upande wa Biashara ambalo lilikataliwa na Mwamuzi wa pembeni kwa kudai kuwa lilikuwa la kuotea huku macho ya wengi wakiamini haikuwa hivyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic