KIUNGO YANGA AACHANA NA SOKA
Aliyekuwa kiungo wa zamani wa klabu ya Yanga na Ndanda FC, Salum Telela, ameachana rasmi na soka la ushindani baada ya kuajiriwa na Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO) kama Mhasibu, imeelezwa.
Telela ameajiriwa na TANESCO huko Mtwara ambapo sasa mchezo wa soka ameuweka kando na badala yake atawajibika na shughuli za uhasibu ndani ya shirika hilo la serikali huko Mtwara.
Kiungo huyo ambaye aling'ara wakati akiichezea Yanga na baadaye Ndanda ya huko Mtwara, alifanikiwa kupata Stashahada ya Uhasibu 'Diploma' katika cha St. Augustine kilichopo Mtwara mwaka 2017.
Ikumbukwe Telela wakati anaondoka Yanga alitangaza kupumzika kwa muda kucheza soka baada ya kuamua kurejea darasani kumalizia masomo yake na baadaye akaamua kuanza kuitumikia Ndanda kabla ya kuamua rasmi kuachana na mchezo wa soka.









0 COMMENTS:
Post a Comment