September 26, 2018



Pamoja na kwamba atamkosa nahodha wake, John Bocco katika mechi dhidi ya watani wake, Yanga wikiendi hii, Kocha Patrick Aussems amefanya naye kikao cha dharura.

Aussems, Bocco pamoja na Emmanuel Okwi walikuwa na muda mchache wa kuzungumza mambo kadhaa wakiwa uwanjani wakati wa mazoezi, leo.

Mazoezi hayo yalifanyika kwenye Uwanja wa Bocco Veterani na Aussems na wachezaji hao walisimama pamoja kwa takribani dakika tano wakijadili jambo.

Kwa pamoja walionekana kuwa watulivu na walizungumza huku kocha huyo raia wa Ubelgiji akionekana kuwa ndiye mchangiaji mkubwa zaidi.

Bocco ataikosa mechi hiyo muhimu kwa Simba baada ya kupambwa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Mwadui FC mjini Shinyanga.


1 COMMENTS:

  1. Yanga wanafurahi sana kutokuwepo kwa boko na kuona kuwa Okwi hana madhara lakini wakumbuke ule mwaka walikula tano bila Mashabiki walimlalamikia sana okwi kuwa kwann huwa aifungi yanga akaja kuwjibu uwanjani kwa kufunga maholi mawili na kutoa assist kwa magoli matatu.So yanga waendelee kujipa moyo okwi hana madhara

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic