September 10, 2018


Baada ya kukiwezesha kikosi cha Taifa Stars kwenda suluhu bila kufungana na Uganda The Cranes, Kocha Mkuu wa timu hiyo Emmanuel Amunike amemwagiwa sifa na Jamhuri Kihwelo 'Julio'.

Julio ambaye ni aliwahi kuifundisha na sasa ni Kocha Mkuu wa Dodoma FC, amesema Amunike ameanza kazi vizuri na ni vema akapewa muda zaidi kuliko kuanza kumkosoa mapema.

Kocha huyo anayependa sifa kuliko pesa, ameeleza kuwa Amunike ni bonge la Kocha hivyo kama akipewa muda ipasavyo anaweza akaifikisha timu mbali.

Aidha, Julio amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa naye bega kwa bega ili kuhakikisha majukumu yake nayaenda vema kuiwezesha Stars kufika mbali.

"Huu ni mwanzo mzuri kwa Stars, Amunike anastahili pongezi na inabidi apewe nguvu na TFF ili kuiwezesha Stars kufika mbali" alisema.

2 COMMENTS:

  1. Nani kocha wa Simba hapo?Mbona mnakuwa waongo..Hii blog ilishakuwa ya udaku.Sikh nyingine tafadhali andika Nina lako tukujue were mwanfishi ni nani unayeandika upuuzi

    ReplyDelete
  2. ungeandika kocha wa dodoma fc watu wasingesoma au hamjui simba inafundishwa na nani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic