September 25, 2018


Luka Modric raia wa Croatia anayecheza soka na klabu ya Hispania ya Real Madrid, amebeba tuzo ya Mchezaji Bora wa shirikisho la soka duniani (Fifa) katika hafla iliyofanyika usiku wa kuamkia leo Royal Festival Hall, jijini London, England.

Mwanasoka huyo amewazidi kete mastaa wengine wa mchezo huo,  Cristiano Ronaldo na Mohamed Salah,  ambapo alishinda pia tuzo ya Golden Ball kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika mwaka huu nchini Russia, na pia alishinda Tuzo ya Mchezaji wa Mwaka wa shirikisho la soka la Ulaya (UEFA).

Modric alikuwemo katika kikosi cha Real Madrid kilichotwaa ushindi wa Ligi ya Mabingwa mwezi Mei mwaka huu na aliiongoza Croatia kufika fainali za Kombe la Dunia iliposhindwa na Ufaransa.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Misri na klabu ya Liverpool,  Salah, ametwaa tuzo ya FIFA Puskas ya goli bora zaidi, hii ni baada ya umahiri wake ambao uliifikisha Liverpool katika Ligi ya Mabingwa.

Golikipa wa Hispania na klabu ya Chelsea ya Uingereza,  Thibaut Courtois,  ametwaa tuzo ya Golikipa Bora wa Mwaka, na kocha aliyeifanikisha Ufaransa kutwaa Kombe la Dunia, Didier Deschamps,  ameshinda tuzo ya Kocha wa Mwaka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic