September 29, 2018


Kuelekea mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga itakayopigwa Septemba 30 2018, Wizara ya Afya nchini imetangaza upimaji wa afya wa hiari kwa mashabiki watakaohudhuria mechi hiyo.

Simba na Yanga zinashuka kesho Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 11 za jioni kuwania alama tatu katika Ligi Kuu Bara.

Kuelekea mechi hiyo, Wizara imesema itakuwa inatoa huduma ya upimaji wa maambukizi ya virusi vya Ukimwi ili kuwawezesha mashabiki hao kujua hali za afya zao.

Taarifa imeeleza kuwa licha ya kupima, huduma nyingine itakayotolewa ni pamoja na uchangiaji damu ambayo itahusika katika kusaidia walio na upungufu kuwaongezea mahospitalini.

Mbali na kuchagia damu, aisha imeelezwa kuwa Wizara hiyo itatoa huduma ya elimu kuhusiana na masuala ya afya kwa ujumla ili kuweka uelewa wa mambo kwa baadhi ya magonjwa.

3 COMMENTS:

  1. Wamefanya jambo jema..japo game kama lile ilikua bora wapimwe watu ambao watakua na presha kubwa...wasije wakaleta balaaa uwanjan...

    ReplyDelete
  2. Aliyekeenda kuona mechi ya watani wa jadi na ili ajifurahishe na akagunduwa kuwa ana ukimwi na siku zake za kuishi zakuhesabika vipi itakuwa
    hali yake?

    ReplyDelete
  3. Hapo sio mahali pake , waende wakapime kwenye matamasha ya fiesta

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic