September 16, 2018


Baada ya kugundua umuhimu na ugumu wa mechi ya Yanga, Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems ameianzia mkakati maalum ikiwemo kumkabidhi majukumu mengi ya mchezo huo, msaidizi wake, Masoud Djuma.

Masoud ambaye ni mzoefu na Ligi Kuu Bara, atakuwepo kwenye Uwanja wa Taifa leo kuangalia mabadiliko ya kiufundi yaliyomo katika kikosi cha Yanga inayocheza na Stand United wakati Simba ikijiandaa kwenda Mwanza.

Simba na Yanga zimebakiza siku 14 kabla ya kupambana kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo Mnyama atakuwa mwenyeji.

Aussems ambaye timu yake ilicheza jana na Ndanda mjini Mtwara, ameliambia Spoti Xtra kwamba ameangalia mchezo wa mwisho wa watani wa jadi lakini amegundua kuna mabadiliko makubwa ya wachezaji haswa kwa Yanga ambayo anahitaji kuyafanyia kazi haraka.

Habari za uhakika zinasema kwamba Masoud hatakuwepo kwenye mechi zote za kanda ya ziwa na atalazimika kuangalia kiumakini kabisa uimara na udhaifu wa Yanga kwenye mechi ya leo na zile mbili zinazofuata dhidi ya Coastal Union na Singida.

Spoti Xtra limedokezwa kwamba Aussems amekaa na timu yake ya ufundi akawaambia kwamba mechi hizo zitatosha kutoa picha ya mabadiliko yaliyopo ndani ya Yanga kwavile zote watatumia mbinu tofauti.

Wachezaji ambao hawapo kwa upande wa Yanga ni pamoja na Obrey Chirwa, Youthe Rostand na Hassan Kessy ambao wote walicheza mchezo ule na wapya ni Herieter Makambo, Feisal Salum, Deus Kaseke. Klaus Kindoki, Jafary Mohammed na Mrisho Ngassa.

Kwa Simba ambaye hayupo ni Laudit Mavugo ingawa kuna maingizo mapya kama Meddie Kagere, Pascal Wawa, Adam Salamba, Marcel Kaheza, Mohamed Rashid na Deogratius Munishi ‘Dida’

“Yanga ina mabadiliko, ambayo niliweza kuiona siyo kama ya sasa lakini kwangu naona hii mechi ni kama mechi nyingine sababu presha kubwa bado inabaki kwa mashabiki,”Aussem ameiambia Spoti Xtra.

Kocha huyo aliongeza kwamba; “Na kwa upande wa kikosi changu wachezaji wapo lakini wengine wameongezeka hivyo huwezi kufananisha na kikosi kile ambacho kiliweza kucheza msimu ule.” alisema.

Masoud alionekana akichukua dondoo kwenye mechi ya African Lyon na Coastal Union na alipoulizwa alisisitiza alikuwa akifanya tathmini ya washindani wake kama sehemu ya kazi ya benchi lake ya ufundi ingawa hakutaka kufafanua zaidi.

CHANZO: SPOTI XTRA

2 COMMENTS:

  1. timu zetu lazimu zibadiliki na kuona umuhimu wa kila mchezo katika ligi. michezo yote ina uzito sawa kwa maana ya pointi. bila umakini nawezakuta michezo yote ile mnayoona rahisi na migumu timu inashindwa kufanya vizuri. tubadilike

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic