September 16, 2018


Mlinda Mlango wa timu ya Yanga, Ramadhani Kabiwli, jana alijikuta akiondolewa kwenye ratiba ya mazoezi baada ya kuchelewa kujumuika na wenzake kwenye mlo wa mchana.

Kabwili aliondolewa na Kocha Mkuu, Mkongomani Mwinyi Zahera kutokana na kushindwa kufuata ratiba ilivyopangwa akieleza kuwa hakuwa na sababu za msingi.

Yanga ilikuwa inaendelea na mazoezi jana kwa ajili ya kukamilisha maandalizi kuelekea kipute dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa Taifa, leo.

Mpaka sasa Kabwili ameshaondolewa kambini kutokana na kuchelewa kwake huko Kocha Zahera akitoa msisitizo wa kuwataka wachezaji wote Yanga kufuata ratiba la sivyo hakutakuwa na cha msalia mtume.

Mechi ya Yanga na Stand United itapigwa leo Uwanja wa Taifa majira ya saa 10 kamili jioni na mechi ikienda mbashara kupitia kituo cha Azam TV.

1 COMMENTS:

  1. Sawasawa kocha nizamu ndogo kama izo ukiweza kuzizibiti basi nizamu kubwa inakuwa rahisi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic