MBELGIJI SIMBA AZITAKA POINTI HIZI DAR, ZIMO ZA YANGA
Patrick Aussems ameweka wazi kwamba mbinu pekee ambayo itaipa ubingwa Simba kwa msimu wa pili mfululizo ni kutopoteza pointi yoyote kwenye mchezo wao ambao watacheza nyumbani na watatakiwa kukusanya pointi 57 ambazo watazigombania.
Kocha huyo raia wa Ubelgiji ambaye tayari ameshaiongoza Simba kwenye michezo miwili ya ligi kuu hadi sasa bado ana kibarua cha michezo 17 ijayo ambayo watakuwa wanaichezea katika Uwanja wa Taifa jijini Dar ambao wamekuwa wakiutumia kama uwanja wao wanapokuwa na michezo ya nyumbani.
Kocha huyo ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Simba ameliambia Championi Jumatano, kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na kufahamu wazi juu ya ugumu ambao watakutana nao kwenye michezo yao ya ugenini ambayo itakuwa kazi ngumu kwao kutokana na kutokuwa na mazingira rafiki ya kuchezea tofauti na vile ambavyo watacheza kwenye Uwanja wa Taifa.
“Siyo mbaya hadi sasa tumecheza michezo miwili hapa nyumbani na tumefanikiwa kushinda yote, hiyo imetokana na jinsi ambavyo tulivyojiandaa vizuri lakini bado tuna kazi kubwa ya kuifanya kwenye michezo yetu inayokuja.
“Unajua kwamba tumeanzia hapa nyumbani na baada ya muda mfupi tutaanza kutoka kwenda ugenini hivyo hili tusiende kupata shida sana huko nimepanga ni lazima kwamba tushinde michezo yetu iliyobakia ya hapa nyumbani ili tupunguze presha pale ambapo tutaanza kwenda huko mkoani kwa sababu naelewa mazingira ya kucheza ugenini kwamba kuna mazingira yasiyo rafiki sana kwa wachezaji kupata matokeo,” alisema Kocha huyo.
Simba itacheza michezo 38 ambapo michezo 19 watacheza kwenye uwanja wa nyumbani na michezo mingine 19 wataicheza katika viwanja mbalimbali wakiwa ugenini vikiwemo Mkwakwani, Tanga na Kirumba, Mwanza.
N kwel tafta points zote home
ReplyDeleteKila timu ina malengo hayohayo
ReplyDeletetunahitaji ushindi hata ugenini tuna kikosi kipana .hakuna haja ya kuitaji ushindi wa nyumbani pekee, nikukaza tu kamaba tu kamba
ReplyDelete