September 1, 2018


Mwananchi mmoja ambaye amejitokeza kwenye mnada wa kununua makontena yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema katika makontena yote 20 hakubahatika kuona masofa ndani yake badala ya viti na samani nyingine.

“Tulipata fursa ya kukagua makontena yote 20 siku chache kabla ya mnada, mimi niseme ukweli tu sikuona masofa kwenye hayo makontena, lakini kuna viti ya cabinet,” alisema mnunuzi huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Ibrahim.

Pia amesema bei iliyowekwa na TRA wao kama wanunuzi hawaijui, huku akidai kwamba ujazo wa makontena hayo ni mdogo. (Yana mzigo kidogo ikilinganishwa na ukubwa wake) na kuongeza kuwa iwapo ikipangwa vizuri yanaweza kutoka makontena matano au sita pekee badala ya 20 yanayotajwa.

Mnada wa makontena 20 ya Makonda umefanyika bila mafanikio, baada ya wateja kushindwa kufika bei ikiwa ni mara ya pili kwa makontena hayo kukosa wateja tangu yalipoanza kuuzwa Agosti 25.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ghala la Dar es Salaam Inland Container Depot (DIC) leo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya udalali ya Yono (Auction Mart), Scholastica Kevela amesema wataendelea na mnada hadi makontena hayo yauzike.

Hata hivyo, Kevela alikataa kutaja bei ya mwisho akisema hiyo ni kazi ya Kamishna mkuu wa Mamlaka ya mapato (TRA). Mbali na makontena hayo, Kevela alisema wameuza bidhaa mbalimbali katika mnada huo na wataendelea nao wiki ijayo.


9 COMMENTS:

  1. Siasa na ushabiki vikishaingizwa kwenye mambo yenye uhalisia huchukua muda mfupi ukweli kudhihiri

    ReplyDelete
  2. Kwa hiyo huyo mnunuzi alienda kununua au kukagua ili atuletee taarifa?
    Je inamaanisha anasuta taarifa zilizotolewa?

    ReplyDelete
  3. ACHENI UMBUMBU UKIENDA DUKANI KUNUNUA SIMU HATAKAMA UNAIFAHAMU SAMSUNG GALAXY S7 LAZIMA UIKAGUE KWANZA,SASA WEWE UNAEJIFANYA UNAMUONA MNUNUZI HAYUKO SAWA POLE SANA,UKIENDA KUOA UNAAMBIWA MKAGUE MKEO KUHAKIKI KAMA NDIYE AU LAAA,IJEKUA KWENYE BIASHARA TENA YA MAMLIONI ACHA UTANI WEWE YUKO SAHIHI,NA NINACHOKIONA MIMI WAZEE WALISHACHAKACHUA SIKU NYINGI SANA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeelewa hoja au ndio umejibu tu kwa mhemko :D :D

      Delete
    2. Maandishi kuyasoma ni jambo moja kuyaelewa ni jambo jingine mkuu. Kontena hazikaguliwi kama gunia la viazi. Kuna jambo linaendelea hapo iko siku litabainika.

      Delete
    3. kuwa mwelewa ndugu yangu....kama huelewi ni vizuri ukaelewa kwa kujifunza.Bidhaa yoyote inayouzwa hasa hii ya mnada inayoongelewa ni lazima mnunuzi aikague kujiridhisha kama bidhaa zilizotajwa na zikamsukuma yeye kutaka kununua na ndio maana wanunuzi huwa wanapewa siku kadhaa kabla kwa ajili ya kukagua mali inayouzwa ili wajiridhishe.....kama yeye alitaka kununua contena lenye sofa utajuaje?

      Delete
  4. Nikimuangalia vizuri huyu jamaa tena kwa mara tatu tatu hivi sura yake kama ya jamaa yaan mbwa kamla mdog... kama sio baba yake mdogo jamaa basi ndugu wakaribu sizonje... pole sanaaa mjomba

    ReplyDelete
    Replies
    1. hela haipimwi kwa uhandsome na kuvaa vizuri bro....jifunze.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic