September 17, 2018


Baada ya kutemwa kambini kwa muda kutokana na makosa ya kinidhamu, Katibu wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali, amemtaka kipa Ramadhani Kabwili kuonesha nidhamu.

Kabwili aliondolewa kwenye kikosi cha Yanga baada ya kuchelewa kuripoti kambini na kukosa mazoezi ya mwisho ambayo timu ilikuwa inajiandaa kucheza na Stand United.

Mara baada ya kupata taarifa hizo, Akilimali aliibuka na kumtaka Kabwili kutambua kuwa bado ni kijana mdogo hivyo ni vema akaachaa na mambo ya kidunia na badala yake apambane kufikia ndoto zake.

Akilimali amemtaka kipa huyo kinda kuwa nafasi aliyoipata Yanga wapo wengi wanaoitamani lakini wameikosa kutokana na kukosa bahati hiyo ambayo ni adhimu.

Aidha, Akilimali amesisitiza ni vema Kabwili akaongeza nidhamu zaidi ili kujiwekea heshima ndani ya timu na uongozi wake maana atafika mbali zaidi.

4 COMMENTS:

  1. Kwasababu sifa nyingi mlizompa kabla ya kumjuwa ndizo zilizomharibu au pia huenda ikawa hajalipwa ada yake ya usajili aliyoahidiwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umekrem kila siku hakuna hela, sifa kila mtu anapewa kijana alifanya vzr kwenye timu ya vijana akasifiwa na kila mtu naona roho imekuuma kwa yeye kuchezea Yanga.

      Delete
  2. USHAURI MZURI WA KUMJENGA MCHEZAJI

    ReplyDelete
  3. Kama wewe Mzee mwenyewe ni mkosaji mkuu wa nidhamu ktk timu yenu unategemea Kabwili awaje?? Panya anatoa ushauri kwa panya mwenzake kuwa asile mahind ghalani.... Hahahha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic