September 17, 2018


Licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Stabd United, mashabiki wengi wa klabu ya Yanga wameutaka uongozi kumfuka kazi kipa wake Mkongo, Klaus Kindoki.

Mashabiki hao wenye hasira (majina tunayo) wameeleza kutofurahishwa na uwezo wake baada ya kuruhusu mabao matatu.

Kitendo cha Kindoki kufungwa mabao hayo ambayo wameeleza kuwa yalikuwa laini, kimewaumiza baada ya kupoteza mvuto wa ushindi wao ingawa wamepata alama tatu.

Kindoki aliweza kuruhusu mabao hayo na kumpa zawadi straika Alex Kitenge ambaye aliondoka na mpira kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Uwezo wa Kindoki umewaweka njia panda mashabiki hao ambao wengi wao wameona hana uwezo wa kuicheza Yanga la sivyo awekwe benchi kwa muda mpaka pale atakapojifunza.

Baada ya ushindi dhidi ya Stand, Yanga sasa wataanza maandalizi ya kujiandaa na mechi dhidi ya Coastal Union ya Tanga ambayo watacheza nayo Uwanja wa Taifa Jumatano ya wiki hii.

3 COMMENTS:

  1. MASHABIKI TUTULIE MPIRA NDIO ULIVYO ZIPO SIKU ZA JUA NA ZIPO SIKU ZA MVUA GOLIKIPA KINDOKI NDIYE KOCHA KAMLETA NA NDIYE GOLIKIPA NAMBA MOJA WA KLABU. AMECHEZA VIZURI TULIPOCHEZA MECHI ILIYOPITA BAHATI MBAYA MECHI HII HAKUWA VIZURI. TUMPE MUDA.

    ReplyDelete
  2. Mpangeni tarehe 30 bakora zitembee.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli waliozoea kuvunja viti na kuja na matokeo wanayopewa na Manara lazima wapigane bakora.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic