September 7, 2018


Na George Mganga

Wakati Stars ikishuka kesho Uwanja wa Nambole kukipiga na Uganda, Katibu wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema kukosekana kwa Kelvin Yondani itakuwa ni pengo kubwa.

Yondani ambaye anaichezea klabu ya Yanga, ameondolewa katika kikosi cha Stars ikilichosafiri kuelekea Uganda kwa ajili ya mechi hiyo ya kufuzu kuelekea AFCON 2019 baada ya kupatwa na majeraha ya mguu.

Mzee Akilimali anaamini kutokuwepo wa Yondani kunawza kukawa pengo sababu ya uzoefu wake lwenye mechi za kimataifa.

Kuumia kwa Yondani kumemfanya Akilimali apatwe na wasiwasi katika safu ya ulinzi wa timu hiyo ambaye amesalia Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

"Sidhani kama safu ya ulinzi itakuwa imara baada ya Yondani kuumia maana amekuwa na uzoefu wa mechi nyingi za kimataifa, lakini ngoja tusubiri mechi itakavyokuwa yawezekana ikawa bahati endapo tukishinda" alisema.

2 COMMENTS:

  1. KATI YA VITU BLOG HII HUNISIKITISHA NI KUMPA MILEAGE HUYO MZEE!!!

    ReplyDelete
  2. Sioni pengo...kuna Aggrey Moris ni mzuri na mzoefu kwa mechi za kitaifa.Kuna kipindi Yondan alikosekana kwenye timu ya Taifa lkn biashara iliendelea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic