September 7, 2018


Wakati ligi ikizidi kuoamba moto, imeelezwa kuwa straika wa kikosi cha Mbao FC, Pastory Athanas amepania kuchukua kiatu cha mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Athanas ambaye aliwahi kuichezea Simba na Stand United, amesema ana imani kubwa ya kumpiku Emmanuel Okwi ambaye alifanikiwa kuwa mpachika nyavu bora kwa msimu uliopita.

Taarifa imeeleza Athanas amesema licha ya straika hatari Simba, Meddie Kagere aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia FC ya Kenya kuwa mbele na mabao matatu, anaami atampiku na kupanda juu yake.

Athanas amefunguka akisema licha ya kuwa amepachika bao moja pekee ndani ya kikosi cha Mbao uhakika wa kuchuana na Kagere upo na ameahidi kuendelea kupambana.

"Ligi ndiyo imeshaanza, hata kama Kagere amefunga mabao matatu, nina uhakika wa kupambana ili niweze kufunga kila mechi na mwisho wa siku niweze kutimiza malengoya kuwa mfungaji bora" alisema.

2 COMMENTS:

  1. Pastors Athanas awapiku Okwi na Kagera kwenye ufungaji magnolia ligi kuu? Labda mpira bwana wanasema lolote linaweza kutokea hivyo tuite muujiza maana popote unaweza kutoka. Ina maana hata Makambo wa Yanga wote nyuma kwa Pastory? Muujiza.

    ReplyDelete
  2. Pastory Athanas awapiku Okwi na Kagere kwenye ufungaji magoli ligi kuu? Labda mpira bwana wanasema lolote linaweza kutokea hivyo tuite muujiza maana popote unaweza kutoka. Ina maana hata Makambo wa Yanga wote nyuma kwa Pastory? Muujiza.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic