September 22, 2018


Msanii wa Bongo Fleva, Faustine Charles ‘Nandy’ anatarajia kuacha kazi ya muziki ifikapo mwaka 2020 na badala yake atajikita kwenye biashara kwani ndiyo kitu anachokipenda.

Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Nandy alisema ndoto yake ni kuwa mfanyabiashara mkubwa Bongo kwani ndiyo yalikuwa malengo yake pindi tu alipoanza kufanya muziki.

“Wakati naanza kufanya muziki nilijiwekea malengo kwamba baada ya miaka mitano niache muziki ili niendeleze biashara zangu, hivyo namshukuru Mungu kwa sababu mpaka sasa nimeshatumia miaka miwili ambayo ni mwaka 2016 na 2017. 

Kwa hiyo utakapofika mwaka 2020 nitaacha muziki, ila siyo kama nitakuwa sitoi nyimbo hapana nitakuwa natoa lakini kwa mwaka mara moja ili niwe napata muda mzuri wa kusimamia biashara zangu,” alisema Nandy.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic