September 22, 2018


Kwa namna ambavyo mshambuliaji Ibrahim Ajibu anavyozidi kuonyesha uwezo mkubwa uwanjani, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema mchezaji huyo kama ataendelea hivyo basi njia ya kwenda kucheza soka Ufaransa ni nyeupe kwake.

Tangu Zahera ajiunge na Yanga mwishoni mwa msimu uliopita, alikuwa hampi Ajibu nafasi kubwa ya kucheza kwa madai kiwango chake kilishuka lakini msimu huu ameanza kwa kasi huku akifunga bao moja na kutoa asisti nne katika mechi tatu alizocheza.

Zahera alisema kuwa, kwa kocha yeyote yule wa hapa nchini au Ulaya ambaye atamuona Ajibu akicheza kwa kiwango cha sasa, hataweza kubeza uwezo wake.

“Nilikuwa nikipata tabu kubwa na Ajibu jambo ambalo kwa sasa nina imani amelifanyia kazi na ameendelea kunielewa hivyo kama atajibidiisha zaidi nadhani atafika mbali sana kwa sababu uwezo wake ni mkubwa kiasi kwamba anapaswa kucheza ligi za Ufaransa au nchi nyingine za Ulaya.

“Katika mchezo dhidi ya Coastal Union alifanya vizuri zaidi ya mich­ezo yote ya nyuma tangu nijiunge na timu hii, hivyo kwa namna ambavyo anaendelea atakuja kuwa lulu ambayo si ya kuishia kucheza tu hapa Tanzania, maana ana kila sifa ya mchezaji wa Ulaya endapo atajituma zaidi,” alisema Zahera.

3 COMMENTS:

  1. Binafsi namtakia kila LA kheri Ibrahimu Ajibu Migomba kwani ni mmoja kati ya nguzo tegemeo ndani ya Dar Young Africans.

    ReplyDelete
  2. Bado Kocha hujamuona vizuri Ajibu hajaanza leo kucheza vizuri. Toka yupo Simba ajibu mchezaji mzuri tu tena wakati ule anafunga magoli mwenyewe

    ReplyDelete
  3. Kocha hajamjua Ajibu.Mchezaji wa kuwaka na kupoa.Msimu uliopita alianza vizuri mara akazimika kama mshumaa .Hajitambui ingawa kipaji anacho .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic