September 23, 2018


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtaka Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo, Revocatus Kuuli, kutoa maelezo ya kusimamishwa kwa mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Simba.

Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Wilfred Kidao, imeeleza kutoa siku tatu pekee wa Kuuli kutoa majibu na pia kutaka kujua kama maamuzi hayo ni ya Kamati ya Uchaguzi kupitia kikao kilichofanyika Dodoma.

Kwa mujibu wa barua hiyo kutoka kwa Katibu Kidao, inaelezea masikito ya TFF kuhusiana na maamuzi yake ya kuamua kusimamisha mchakato wa uchaguzi Simba bila ya kuwa na mamlaka pia kushirikiana na TFF.

Aidha pia barua hiyo inataka kujua imekuwa vipi Kuuli asimamishe mchakato wa uchaguzi huo na kwa kupitia kikao kipi kilichojadili hilo suala na kuamua kufanya maamuzi hayo.

Ikumbukwe hivi karibuni Kuuli aliibuka kwenye Vyombo vya Habari akitangaza kuusimamisha mchakato wa uchaguzi wa Simba ambao hivi sasa upo kwenye hatua ya usaili na mpingamizi yakiwa yanaendelea.

Simba inaendelea na zoezi la mapingamizi kwa wanachama wake kabla ya kampeni kuanza na kujiandaa kwa uchaguzi mkuu utakaofanyika Novemba 3 2018.

3 COMMENTS:

  1. Watu wanajiamulia ili kuleta mitafuruku ili kuwakatisha tamaa wawekazaji katika klabu.Hizi ni hujuma dhahiri ambazo hazipaswi kuacha kuchukua hatua kali za kuzikomesha.

    ReplyDelete
  2. Kina "championi"wapo wengi.Hivi unadhani uwekezaji Simba unapendwa na wote?Kuna mahasidi wengi lakini "We shall overcome"Inshallah.

    ReplyDelete
  3. Huyo jamaa ni wakala wa Yanga alietumwa kuikoroga Simba hovyo kabisa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic