SAMATTA AFUNGUKA KUHUSIANA NA WACHEZAJI SITA SIMBA WALIOTEMWA STARS
Na George Mganga
Nahodha wa kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars' Mbwana Samatta, amesema hakuna haja ya wadau wa soka kuanza kuzungumzia wachezaji walioachwa na Kocha wa timu, Emmanuel Emmanuel na badala yake wanapaswa kuweka akili kuelekea mechi dhidi ya Uganda.
Samatta ambaye ndiye Nahodha Mkuu wa kikosi hicho, ameeleza kuwa kutolewa kwa wachezaji hao na Kocha Amunike haina maana ya kuwa si sehemu ya timu, bali wataendelea kuwa pamoja kwa kipindi chote.
Samatta ameamua kuzungumzia hilo kutokana na wachezaji 6 wa klabu ya Simba kutemwa na Kocha Amunike baada ya kuchelewa kuripoti kambini tofauti na muda uliokuwa umepangwa.
Licha ya kuchelewa, Amunike aliwasamehe wachezaji hao baada ya kukutana nao na akawaahidi kuwarejesha tena pale watakapomshawishi kwa kupambana kupitia klabu yao.
Stars inaondoka leo kuelekea kampala, Uganda ampao itacheza mchezo wa kufuzu kuelekea AFCON dhidi ya The Cranes, Septemba 8 2018.








huu mjadala ulishafungwa, tusubiri mechi tuuu now tujadili wachezaji waliopo Stars,msigombanishe watu, mnafikiri ataongea kama SABATO kuhusu Bocco?
ReplyDeleteheeeh heeeh heeh!!!!!.......naona sabato amekufanya povu likutoke bro.by the way kwa kumbukumbu yangu hakumwongelea bocco,alieleza tofauti ya kiwango cha kagere na makambo........labda kama aliongea issue nyingine tena tofauti na hiyo.
Deleteendelea kuipitia hii blog mara kwa mara,unapitwa na vingi,weka bando la mwezi(jokes)
Delete